MWANADADA STARA THOMAS AAMUA KUOKOKA NA KUIMBA NYIMBO ZA INJILI
Mwanamuziki nyota wa kizazi kipya,Stara Thomas hatimaye ameamua kuachana na muziki huo wa kidunia na kuamua kuimba nyimbo za injili.
Stara alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba,Stara alitoa nyimbo zake mbili za mwanzoni zilizokuwa kwa lugha ya kiingereza wimbo wa Children's Right na miaka miwili baadaye alitoa wimbo wa My body,Stara alianza kutamba mnamo mwa mwaka 2000 ambapo alitoa vibao kadhaa kwa lugha ya kiswahili kama vile,Sikia,Mimi na wewe,na nyuma sintorudi.Mwaka 2003 alishinda tuzo ya Best Female Vocalist in Tanzania.
Stara Thomas ni mama wa watoto wawili na pia aliwahi kutamba na vibao mbalimbali akishikiriana na wanamuziki mbalimbali akiwemo K. Basil naye aliyempokea Yesu na kugeukia kuimba nyimbo za Injili.Wimbo mwingine alioshirikishwa na wimbo huo kutamba katika redio na vituo vya Luninga nchini Tanzania ni wimbo wa nipigie alishirikishwa na mwanamziki AT ambao ulitoka mnamo mwaka 2010.Umaarufu wake unatokana na uzuri wa sura yake lakini pia ni sauti yake nzito iliyobarikiwa.
Sikiliza hii hapa kisha utakubaliana nami.
Mungu akubariki sana kila la kheri....
Christina Shusho, Upendo Nkone na Stara Thomas |

No comments:
Post a Comment
COMMENT HERE: