Slide

Monday, May 23, 2011

Ronald Rubinel Je m'Edith Hommage à Edith Lefel ( zouk 2003)

Mnamkumbuka mwanamama huyu??????

November 1963 ndiyo siku aliyozaliwa mwimbaji Edith Lefel kutoka French Guyana,alizaliwa Guyana na kukulia  Martinique,alikuwa maarufu sana kwenye nyimbo zenye mahadhi ya Zouk-love,Kipaji chake kilichomoza mnamo mwaka wa 1984 akiwa anafanya kazi na Jean-Michel Cabrimol's group Maffia,mnamo mwaka wa 1987 Edith aliweza kufanya kazi na kundi maarufu la Malavoi pia amewahi kushirikiana na waimbaji mbalimbali,Edith alibahatika kupata watoto mapacha na producer maarufu wa kifaransa Ronald Rubine.Alitamba na vibao kadhaa kikiwemo  Fanm .Album yake ya mwisho kuitoa ilikuwa mnamo mwak 2002,Mnamo January 20,2003 akiwa na umri wa miaka 39 aliaga dunia,alilala na hakuamka tena sababu za kifo chake zilichangiwa na uvutaji sigara na utumiaji wa dawa za uzazi wa mpango.Alizikwa katika makaburi ya watu maarufu huko katika jiji la  Paris.
Hili ndio kaburi lake